Sunday, December 23, 2012

WIMBO MPYA WA KANDINDI HEWANI

Baada ya kimya cha zaidi ya miaka mitatu mwanamuziki nguli wa miondoko vionjo vya kikwetu a.k.a BONGO BEAT Che Mundugwao ameibuka na wimbo mpya funga mwaka 2012 unaoitwa Kandindi(kandege) na utaanza kusikika tarehe 28/12/2012, katika vituo vya radio hapa Tanzania na natumaini itakata kiu kwa washabiki wake wa miondoko hiyo. hapa ni sehemu tu ya tafsiri ya wimbo huo ambao umeibwa sehemu kubwa  lugha ya Kiyao wanaotokea kusini mwa Tanzania Mkoa wa Mtwara wilaya ya Masasi jimbo la Lulindi. 
sikiliza na download hapa

KANDINDI
KANDINDI NI JINA NENO LA JINA LA KIYAO LA NDEGE ANAEITWA KING FISHER. NDEGE HUYU ANA UMBO DOGO LENYE RANGI YA KAHAWIA, NA SAUTI NZURI, ANAPATIKANA HAPA KWETU NA AFRICA KWA UJUMLA.
HUYO NDIO KANDINDI  ALIYEBEBA JINA LA WIMBO MPYA MWANAMUZIKI NGULI WA VIONJO VYA ASILI CHE MUNDUGWAO (MTOTO WA LULINDI) AMBAYE AMETOA DECEMBER 2012 BAADA KIMYA CHA MIAKA 2
WIMBO PIA UNAZUNGUMZIA MAISHA KWA NYAKATI TOFAUTI KILA WAKATI NIKIWA NAENDA NYUMBANI KULE KIJIJI CHA LULINDI WILAYA MASASI,MAMAYANGU ALIKUWA AKINIIMBIA MARA KWA MARA BETI HIZI


UBETI WA 1
 KANDINDI KANDINDI- KANDINDI KANOKOTE (KANDINDI KAMCHUKUE/KAMUOKOTE) X 4
MWASOSANGA LEO AICHE APANO (ULIYEMTAFUTA LEO KAFIKA HAPA) KWA MAANA MTU MLIYEPOTEZANA NAE MIAKA MINGI SIKU YA KUONANA LAZIMA MFURAHI PAMOJA
( kuna wakati nililkuwa sijafika pale lulindi miaka mingi Mama na Bibi yangu alivyoniona akaniimbia )

-ANYA BABA ANYA MAMA MKWALOLA ACHE MUNDUGWAO LEO ACHE MBELEMENDE KUNONG’A: KINA BABA KINA MAMA UNAMUONA CHE MUNDUGWAO LEO TUJUMIKA PAMOJA   MBAAZI tamu (mbaazi nazipenda sana tangu utoto)

UBETI 2: MWATIJI NGAIKA -AICHE LELO (MLISEMA AFIKIAMEFIKA LEO)
 HII ILINICHUKUA TENA MUDA MREFU SIKUFIKA NYUMBANI NILIKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA FAMILIA YANGU MANENO HAYA YALILETA MAANA KATIKA MATUKIO HAYO
PETANDA PO PANAGWENA JIKUTINDIULA NDOMONDO NKATI MESI- MBAGWE MBAGWE
PALE PEMBENI KUNA KIBOKO LAKINI NDANI YA KISIMA KATIKATI YA MAJI KUNA MAMBA ANATIBUA MAJI

UBETI WA MWISHO
KINAMAMA -NTENDE YEILA, KINABABA NAVIJANA,-NTENDE YEILA –YEILA (fanya mpango nipatie panya)
KWA ASILI NENO YEILA NI PANYA NI UKWELI USIPINGIKA BAADHI YA MAKABILA  YA KUSINI  WANAKULA PANYA LAKINI NI PANYA WALE WANAOPATIKANA SHAMBANI NASIYO PANYA WANYUMBANI,KUNA TOFAUTI AINA YA PANYA
SHAABAHA YANGU KUINGIZA UBETI HUU KUWAKUMBUSHA MAMBO MENGI ENZI HIZO NA SEHEMU YA MAISHA YA ZAMANI NAMNA WALIVYOWEZA KUSHIRIKIANA KWA UPENDO WATU WA JAMII HIYO

KANDINDI(KANDEGE) WIMBO WENYE VIONJO VYA NGOMA ZA LIKWATA NA SOGEA AMBAYO UCHEZWA WA WATU WA JAMII YA WAYAO NA KUCHANGANYWA NA MIDUNDO YA KISASA+KIKWETU=BONGO BEAT.
WIMBO WENYE MKUSANYIKO WA MATUKIO YATOKEA MIAKA YA NYUMA KUYALETA PAMOJA MADHUMINI KUWAKUMBUSHA MAMBO YA KALE NA KUHIFADHI HISTORIA KWA NJIA MBADALA YA MUZIKI

Washiriki:
 Lead vocal, arranger: Che Mundugwao
 Back vocals: Haris Nyato, Ngaikosya, Manea Mundugwao
 Keyboard/guitar &arranger – Geofrey Kumbulu
 Bass guitar -Mohamed Mgolo
 Drum/njembe-Mr.Kauzeni
 Conga/filimbi – Che Mundugwao
 Percussions- Geofrey Kumbulu
 Studio: Juliet Recordings, Producer: Geofrey Kumbulu

MIMI CHE MUNDUGWAO NAWATAKIA KILA LA KHERI WALE WOTE WAAMINIO SIKUKUU YA X MAS NA MWAKA MPYA 2013.

    

No comments:

Post a Comment